BREAKING: Beki wa pembeni wa Simba, Shomari Kapombe amesaini dili jipya baada ya kukubaliana na uongozi kuongeza mkataba.
Beki huyo mzawa chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes mkataba wake ulikuwa unafika ukingoni mwishoni mwa msimu wa 2020/21.
Alikuwa anatajwa kuingia rada za FAR Rabat ya Morocco pamoja na timu nyingine nchini Afrika Kusini ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake.
Baada ya makubaliano mazuri na mabosi wake wa sasa nyota huyo amesaini dili jipya na inaelezwa ni kandarasi ya miaka miwili.
Kazi na iendelee
ReplyDeleteGazeti lako liliandika anasepa aibu yako bro
ReplyDeleteGazeti lako liliandika anasepa aibu yako bro
ReplyDeleteMnyama anafanya bila ya haraka au papara kwa kujuwa kuwa hapana atayethubutu kuwaota mastaa wake na hata wale wanaojaribu hufanya kwa siri na kuona haya wakijuwa si kiasi chao
ReplyDeleteAnasaini huku uso wake umejaa furaha na tabasamu
ReplyDelete