April 30, 2021


 UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa hawapo tayari kumuuza staa wao, Mzimbabwe, Prince Dube, kwenda Simba na badala yake ataendelea kubaki kikosini kwao.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za Simba kuwa kwenye mipango ya kumnasa mshambuliaji huyo anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu Bara akiwa amepachika 12.

 

Taarifa zilizopo kwa sasa ni kwamba, hivi karibuni mshambuliaji huyo ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Azam, hivyo atakuwa hapo hadi 2024.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema Dube hataenda timu yoyote hapa nchini, bali atabaki Azam.

Popat aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo kama akiondoka Azam, basi atakwenda kucheza soka nje ya Tanzania.


“Kwa kifupi Dube hatakwenda popote ndani ya nchi hii, ataendelea kubaki Azam.

 

“Dube kama akiondoka hapa Azam, basi atakwenda kucheza soka nje ya Tanzania na siyo kwenye klabu za hapa.

 

“Hizo timu zinazomtaka hata watoe dau kubwa kiasi gani, sisi Azam hatutalipokea, hivyo nao waende kutafuta wachezaji bora nje ya nchi kama sisi tulivyokwenda kumtafuta Dube,” alisema Popat.

4 COMMENTS:

  1. Kwa hiyoh na nyie hamtasajili kutoka timu za ndani, au roho mbaya tu

    ReplyDelete
  2. Huo sasa ni ujuha, kama mnaweza kumruhusu kwa timu za nje kuna shida gani kuziuzia timu za ndani kama zirafika bei? Ukisikia kuumiza mpira wa Tanzania ndio vituko kama hivi. Timu yoyote ya Tz ikifanikiwa sifa ni yetu sote kama nchi acheni ujinga wa kizamani. Mnaona leo Tz inapewa nafasi 4 kwa ajili ya juhudi ya vilabu

    ReplyDelete
  3. Inaonesha Azam inachukuwa mkondo wa Yanga dhidi ya Simba. Aliepewa kapewa bwanaaa

    ReplyDelete
  4. Kwa hakika sikutegemea kusikia kauli tata iliyotolewa na Popat kama hii. Isije ikawa imetolewa na mtu asie familia ya mpira wetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic