April 16, 2021

 


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wameamua kuwaengua mastaa wa kikosi hicho ambao hawana mchango mkubwa katika kikosi hicho ili kufanya usajili mpya.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zimeeleza kuwa tayari baadhi ya wachezaji wameanza kupewa taarifa kwamba hawataongezewa mikataba pale ambapo msimu utakwisha.

Kwa sasa Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi 51 kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 huku watani zao wa jadi Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 49 wamecheza mechi 21.

Mtoa taarifa huyo amesema:"Kuna wachezaji ambao wameambiwa kwamba hawataongezewa mikataba pale muda wao ukiisha miongoni mwao ni pamoja na Fiston Abdulazack ambaye hajawa kwenye ubora wake.

"Pia Michael Sarpong huyu naye kuna hatihati akaachwa kwa kuwa nafasi yake imezidi kuwa ndogo kikosi cha kwanza na hafungi mabao kama ilivyo kazi yake, yule Muangola, (Carlos Carlinhos) amebadilika hivyo akiendelea kuwa hivyo atakutana na adhabu pia.

"Orodha ni ndefu na panga ambalo litapita ni kubwa ukitazama Wazir Junior, Farid Mussa hawa kubaki itakuwa ngumu, Ditram Nchimbi huyu bado wanamtazama kwa kuwa amekuwa na mchango kiasi chake licha ya wengi kumlalamikia kwamba hafungi.

"Lengo la kufanya hivi ni kuboresha kikosi na juzi mabosi walikutana kujadili namna ya kufanya maboresho ya kikosi cha Yanga," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema kuwa wanatarajia kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana kutokidhi mahitaji.

5 COMMENTS:

  1. Nawashauri Utopolo kuwa Farid Musa aendelee kubaki

    ReplyDelete
  2. muandish wa habari hii ni kiazi kweli,heading inasema Mastaa yanga kupigwa chini mazima...ukisoma kiundani unakutana na neno KUNA HATI HATI AKAACHWA...Ina maana hauna unachokijua na wala hujui unaandika nini....HUU NI MSIBA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Exactly this is what i was noticing,i guess something is missing. Anyways if you need any help regarding academic life then essay writing Pakistan is the go to way! we make sure that the assignments are all returned on time and at high-quality level. The team members at cheap assignment UK provide you with the best quality content assignment as per your demand. So, if you need any help regarding your assignment writing then cheap assignment is the writing service to turn to.

      Delete
  3. Hao kuuvunja mkataba yao itabidi walipwe mikanja mikubwa

    ReplyDelete
  4. Msifanye makosa kama mulivyokosea kumtema Dilunga tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic