April 16, 2021


 VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania.

Ikiwa ipo nafasi ya tatu na pointi 47 baada ya kucheza michezo 25 inakutana na JKT Tanzania iliyo na pointi 27 baada ya kucheza mechi 25.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kwa kuwa Azam inawania taji la ligi huku JKT Tanzania ikipambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja.

Bahati amesema:"Wachezaji wapo vizuri na tulifika salama Dodoma tukitokea Dar hilo ni jambo jema na tunaamini kwamba tutafanya vema mchezo wetu.

"Kazi ambayo imebaki kwa wachezaji kukamilisha kile ambacho tumekuwa tukifanya kwenye mazoezi wakati wa maandalizi," amesema.

Mchezo wa leo utachezwa Uwaja wa Jamhuri, Dodoma majira ya saa 8:00 mchana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic