April 16, 2021

 


KIWANGO cha juu ambacho anakizidi kukionesha kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, kimekuwa bora kiasi kwamba kwa sasa anawakimbiza Waarabu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kiungo huyo anawakimbiza nyota hao wa Kiarabu kwenye suala la ufungaji kwenye michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo hadi sasa ikiwa imekamilika hatua ya makundi, tayari amefunga mabao matatu.

 

Raia huyo wa Msumbiji, yupo sambamba na nyota wa Wydad Casablanca ya Morocco, Ayoub El Kaabi, Mohamed Ali Ben Romdhane (Espérance ya Tunisia), Amir Sayoud (CR Belouizdad ya Algeria) na Mohamed Sherif (Al Ahly ya Misri) ambao wote hao ni vinara wa kuzifumania nyavu.


Luis anawakimbiza nyota hao kwa kuwa mabao yake yameisadia Simba kufuzu kibabe hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ikiwa na pointi 13, baada ya kushinda mechi tano, sare moja na kupoteza moja tofauti na mastaa hao wengine kwenye timu zao.


Mabao hayo aliyafunga dhidi ya Al Ahly, AS Vita na Al Merrikh, yote Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Luis katika hatua ya makundi, amehusika kwenye mabao sita akifunga matatu, asisti mbili alizotoa kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh na AS Vita, zote ilikuwa Uwanja wa Mkapa akiwapa Chris Mugalu na Clatous Chama.Pia akasababisha penalti moja iliyofungwa na Mugalu katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita, ugenini.

 

Simba ikiwa imetinga robo fainali ya michuano hiyo ikiongoza Kundi A, kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na timu moja kati ya CR Belouizdad ya Algeria, MC Alger (Algeria) na Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) ambazo zimeshika nafasi ya pili kwenye makundi yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic