April 1, 2021


 FROLENT Ibenge, Kocha Mkuu wa Klabu ya AS Vita ambaye pia anainoa timu ya taifa ya DR Congo ameambulia majanga kwenye timu yake ya taifa baada ya timu hiyo kufungashiwa virago kuwania kufuzu Afcon.

Licha ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Gambia kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Martyrs. Aprili 3 ana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

Ni Kazadi Kasengu alipachika bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45+2 na kuipa pointi tatu muhimu timu yake.

Kwenye kundi D, DR Congo imekusanya jumla ya pointi 9 ikiwa imecheza mechi 6 ilishinda mechi mbili, sare tatu na ilipoteza mchezo mmoja.

Timu ambazo zimefuzu kushiriki Afcon nchini Cameroon ni pamoja na Gambia na Gabon ambazo zimekusanya kibindoni jumla ya pointi 10.


Ibenge amesema kuwa ratiba za maandalizi zimekuwa ngumu jambo ambalo linampa kazi kubwa ya kufanya ila anaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

7 COMMENTS:

  1. huyu kocha atafukuzwa siku sio nyingi akifungwa tu na Simba kibarua kinaota nyasi...

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio rahisi hvyo anapendwa sana kwao huyo jamaa

      Delete
  2. Maelezo ya muandishi hayaeleweki

    ReplyDelete
  3. Waandishiiii mnatuchanga tunguzen ukali wa maneno

    ReplyDelete
  4. Upumbavu mtupu,taaluma imevamiwa.

    ReplyDelete
  5. sasa kocha anashinda we unaandika majanga kweli akili hamna

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawe uelewa wako mdogo, sikafeli kufuzu Afcon

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic