April 28, 2021


BEKI wa kati wa klabu ya Simba, raia wa Kenya, Joash Onyango amesema kwa sasa bado hajapata taarifa yeyote kuhusu yeye kuhitajika na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

 Hivi karibuni imekuwa ikielezwa kuwa beki huyo yupo kwenye rada za mabosi wa timu ya Afrika Kusini wakihitaji kupata saini yake.


Kuhusu suala hilo Joash Onyango amesema; “Bado sijapata taarifa zozote kuhusu hilo.”

 

Tokea ajiunge na kikosi cha Simba mwanzoni mwa msimu huu, Onyango ameoneha kiwango bora na kuwa mlinzi chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes 


 

Onyango amefunga bao moja kwenye ligi kuu bara tena likiwa ni la kuisawazishia Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kuufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1 na kutengeneza nafasi moja ya bao kwa kumpasia John Bocco aliyefunga bao pekee dhidi ya klabu ya Mwadui.

3 COMMENTS:

  1. Onyango piga kazi umeshawazima waliokuwa wanakubeza. No wonder hata marefa juzi juzi walikufanyia mtimanyongo kukunyima bao halali ungekuwa nayo mawili sasa

    ReplyDelete
  2. Pumbavu nyie wandishi, mbona kila siku nyie wenyewe ndo mlikiwa mnaandika hayo

    ReplyDelete
  3. Uzushi tupu nani SA atachukua kiroba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic