April 5, 2021

 


BAADA ya kuongoza kikosi chake kutinga hatua ya robo fainali, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji pongezi kwa kufikia malengo hayo.

Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita kwenye mchezo wa tano uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 3 umewapa tiketi ya moja kwa moja kutinga hatua hiyo wakiwa na pointi 13.

Mchezo wao wa mwisho ni dhidi ya Al Ahly ambayo ipo nafasi ya pili na ina pointi mbili, huku AS Vita ikibaki na pointi zake nne na A l Merrikh wao wana pointi 2.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa ni muhimu kuwapa pongezi wachezaji kwa kuwa wamekuwa wakitimiza majukumu yao kwa wakati.

"Wachezaji wanahitaji pongezi kwa kuwa wanafanya jitihada kubwa kila wakati katika kusaka ushindi na ni furaha kwetu kuona kwamba kila mmoja anafanya hivyo.

"Bado kazi ipo na nina amini kwamba kila mmoja anajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo na wao watapambana kuyatafuta," amesema.

Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda bao 1-0 lilifungwa na Luis Miquissone kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama.

2 COMMENTS:

  1. Jisahihishe hapo. Al Ahli sio yenye pointi mbili, yenye pointi mbili ni Al Marikh ambayo ilijaribu kutaka pointi za mezani kutoka kwa Mnyama lakini wakawejwa pembeni

    ReplyDelete
  2. Tulishasema hapa hapa, kwamba simba na AL AHLY wanakwenda ROBO, na utopolo watapata ticket mwakan kwa hisan ya mnyama,vita anacheza mpira ila ni rahis sana kusomwa mbinu zake na timu pinzani, ndiomana AHLY ameweza kumchapa KWAKE, na hata mechi ya mwisho anaweza achapwe tena.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic