April 5, 2021


 WAKATIaliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akitajwa kurejea kwenye klabu hiyo, wachezaji wa zamani wa timu hiyo wamefunguka kuhusiana na ujio wake.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu taarifa zisambae za ujio wa bosi huyo aliyeifanyia Yanga mengi makubwa kipindi cha utawala wake akiwa mwenyekiti.

 

Manji amezua hofu kwa mashabiki wa Simba kutokana na ujio wake huku akiwa na rekodi kubwa ya kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo 2014–15, 2015–16 na 2016–17.


Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa, kwake amezipokea kwa furaha taarifa za ujio wa Manji ndani ya Yanga.

 

Cannavaro amesema kuwa lipo wazi kati ya viongozi waliopita kuiongoza timu hiyo, Manji ni mmoja wapo kutokana na utawala bora aliokuwa nao.


“Hizo taarifa sidhani kama ni kweli, kama ni kweli basi ninaamini ile Yanga ya vikombe inakuja katika misimu ijayo na hilo linawezekana kwake.

 

“Manji alitengeneza kikosi bora kilichochukua ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo na Ngao ya Jamii katika utawala wake tukiwafunga Azam FC pale Uwanja wa Mkapa.

 

“Na mafanikio yake yametokana na usajili bora aliokuwa anaufanya katika timu, kiukweli taarifa hizo nimezipokea kwa mikono miwili na nitampigia simu kuthibitisha hilo kwani namba yake ninayo,” amesema Cannavaro.

 

Alipotafutwa kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athumani Idd ‘Chuji’ kuzungumzia hilo, alisema kuwa: “Kwangu naona faraja kubwa kwa Wanayanga waliokuwa wenye ndoto za timu yao kuchukua ubingwa.

 

“Sijajua lini anakuja huyo Manji, lakini kwa mimi ninayemjua basi Wanayanga watarajie kuona usajili bora wa kisasa ukifanyika utakaoendana na hadhi ya Yanga.

 

“Mimi ninamfahamu vizuri Manji, kwani katika utawala wake nilikuwa sehemu ya wachezaji tegemeo, vitu vyake alikuwa akifanya kwa uwazi na siyo mgumu kutoa fedha yoyote ya usajili ili afanikishe usajili pamoja kambi nzuri," .


Naye mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mohammed Hussein ‘Chinga One’ alisema kuwa: “Sijajua Manji atakuja kukaa nafasi gani, uongozi, mwanachama au vipi, lakini kwangu ninamkaribisha Yanga.


“Ninaamini kama akija ataungana na wadhamini wengine katika kufanikisha mengi mazuri, hakuna asiyemjua Manji kutokana na kukumbukwa na mengi.”

9 COMMENTS:

  1. Wazee wa propaganda hao utopolo fc

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi kwa nini Manyau nyau mkimsikia Manji mnakosa amani?

      Delete
    2. Sisi SIMBA hatuna hofu yoyote juu ya ujio wa Yusufu Manji (kama kweli anarudi). Kwa vyovyote vile hataweza kuifikisha Utopolo hatua ambayo Mnyama ameifikia. Kwanza tujiulize kilicho muondoa ni kitu gani?

      Delete
    3. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepanga kuja na muongozo mpya wa usimamiaji wa vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 kutokana na changamoto nyingi zilizoibuka katika mashindano yake mbalimbali inayoyasimamia.;

      Delete
  2. Karbu tena yusuph manji jangwani

    ReplyDelete
  3. Msitukane mamba kabla hamhavuka mto. Maneno hayo juu ya ujio wa manji yanaimpact gani kwa gsm? Akiwatosa kabla ya huyo manji hali itakuwaje? Taratibu wajemeni

    ReplyDelete
  4. Hayo yanaweza kabisa kuwa na tafsiri kuwa GSM ndie ambae aliekwisha kujitolea na kuendelea kujitolea mabilioni hana thamani na badala yake kuthaminiwa yule ambae amejiondoa na hakuna hakika yoyote kuwa atarejea na hivo nill ndoto ambayo mnaisadiki na baadae kujikoroga kwa vitendo vya kubomoa. Ni bora kujithamini mlichokuwa macho mkononi kuliko kile mnachokiota usingizini

    ReplyDelete
  5. Manji hakujiondoa mwenyewe ila mizengwe na manyanyaso ya bwana fulani na baba'ke ndo yalisababisha akajiondoa katika shughuli mbalimbali ili kumdhoofisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sahihi kabisa, kuna Viongozi wa siasa walimdhalilisha sana.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic