April 25, 2021

 


BAADA ya Jumanne ya Aprili 20, wiki hii Yanga kushusha 
makocha wawili wapya kwa ajili ya kuinoa timu hiyo, ikumbukwe kuwa Alhamisi ya Aprili 22 pia ilimshusha kocha mpya wa viungo, Jawadi Sabri ambaye baada ya kutua nchini aliahidi neema kibao kwa klabu hiyo.

Sabri mwenye uraia wa Morocco ana masters ya

fitness ametua Yanga kuchukuwa nafasi ya Mghana,

Edem Mortotsi aliyedumu kwa kipindi cha muda wa

mwaka mmoja kama kocha wa viungo wa timu hiyo.


Tayari kocha huyo ameanza kazi Kigamboni akiwa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye leo ana kibarua cha kuingoza timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.


Kocha huyo amesema kuwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ni furaha kwake atatumia uzoefu wake kufanya kazi kwa vitendo na kushirikiana na wengine.


“Nafuraha kuona nakuwa sehemu ya kikosi cha

Yanga kwani ni moja kati ya timu kubwa barani

Afrika yenye mashabiki wengi wanaohitaji mafanikio makubwa katika mpira wa miguu. Mimi na

wenzangu naamini tutashirikiana kuhakikisha

tunakamilisha hilo, ” alisema kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic