April 4, 2021


 WAPINZANI wa Klabu ya Namungo leo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Nkana FC wamegoma kufanyia mazoezi ya kupasha misuli ndani ya Uwanja wa Mkapa na badala yake wamefanya nje.

Nkana FC inatarajiwa kumenyana a Namungo FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00.

Timu zote kwenye kundi lao D hakuna ambaye amevuna pointi kwenye mechi mbili ambazo walicheza kwa sababu walipoteza hivyo leo wanaanza upya kusaka pointi.

Wakati walipokuwa kwenye maandalizi ya mchezo huo jana, Kocha Mkuu wa Nkana FC, Kelvin Kaindu alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic