April 6, 2021


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 10.

 Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, KMC ipo nafasi ya tano baada ya kucheza jumla ya mechi 24.

Inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 50 na imecheza jumla ya mechi 23.

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo unatarajiwa kuwa mchezo wenye ushindani ndani ya dakika 90.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari na wanahitaji ushindi.

"Maandalizi yapo vizuri na leo kikosi asubuhi kimefanya mazoezi Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo wetu.

"Utakuwa n mchezo wenye ushindani na imani yetu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwani kikosi kipo imara na wachezaji wana morali kubwa," .

1 COMMENTS:

  1. KMC Amna kazi nyie domodomo tuh siyo kwa yanga ya benchi jipya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic