May 15, 2021

 


JOHN Bocco, nahodha wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kushinda mbele ya Kaizer Chiefs.

Simba leo inatarajia kutupa kete yake kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs saa 1:00 usiku na ule wa marudio unatarajia kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Bocco alisema kuwa wachezaji wamekubaliana kwa pamoja kusaka ushindi mbele ya Kaizer Chiefs ili kuwapa furaha mashabiki pamoja na kufikia malengo ya timu.

“Kaizer Chiefs ni timu bora ndio maana ipo kwenye mashindano ambayo sisi tupo lakini ssi wachezaji kwa pamoja tumekubaliana kupata ushindi kwenye mchezo wetu ili kuyafikia malengo ya timu.

“Hatua ya robo fainali ni ngumu na ina ushindani mkubwa hivyo haitakuwa kazi rahisi kupata ushindi ila tupo tayari na hatutawaangusha Watanzania,” alisema Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic