BAADA ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga kupelekwa mbele kikosi cha Yanga kimewasili uwanjani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.
Muda wa awali ulipangwa saa 11:00 ila taarifa ambayo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imepeleka mbele muda mpaka saa 1:00 usiku.
Wachezaji wa Yanga wameanza mazoezi na wameweka wazi kuwa ikifika dakika 15 watawasubiri wapinzani wao ili kuona kama Simba watafika au la.
Baada ya kumaliza kufanya mazoezi mepesi, kikosi cha Yanga kimerejea ndani huku kikosi cha Simba kikiwasili uwanjani wakati huu.
Pia baadhi ya mashabiki wameanza kutoka uwanjani kwa maelezo kuwa wameshindwa kwenda na wakati.
Nzuri kabisa wameena mambo yapo vibaya kwao na ili kuepuka na aibu ndio wagomee na Mnyama apewe tatu za mezani. Kama kweli mashujaa basi kweli wagomee
ReplyDeleteMikwara mbuzi. Kama wanagomea wagomee kweli.Sio waje kukubali huku wameshawaathiri wachezaji kisaikolojia.
ReplyDeleteSafisana yanga
ReplyDeleteMoira unaendeshwa kwa kanuni na taratibu
ReplyDeleteSafisana yanga
ReplyDeleteHii TFF inadhihirika sasa walimfungia Mwakalebela kwa uonevu. Kwani inaonesha hakuna weledi bodi ya ligi wala TFF yenyewe wanaendesha mambo kikanjanja. Vema bodi ya ligi na uongozi wa TFF wawajibike na kujiuzulu pia ili kuondokana na upuuzi huu.
ReplyDelete