May 29, 2021


 BAADA ya kuondoka Yanga misimu miwili iliyopita, beki wa pembeni, Hassan Kessy, anatajwa kuwa mbioni kurejea kwenye kikosi hicho kwa mara nyingine tena.

 

Taarifa za ndani kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa Kessy anatazamwa kuja kuwa mbadala wa Shomari Kibwana ambaye amekuwa akicheza kwenye nafasi ya beki wa kulia msimu huu.


Mtoa taarifa huyo aliliambia Championi Ijumaa kuwa: “Uongozi upo kwenye mpango wa kumpa mkataba mpya Hassan Kessy kwa ajili ya kuja kucheza kama namba mbili akisaidiana na Kibwana.

 

“Uongozi unamtaka Kessy kwa ajili ya mashindano ya kimataifa msimu ujao, kilichofanya wamtazame yeye ni kwa sababu ana uzoefu wa mechi za kimataifa akiichezea Nkana The Red Devils ya Zambia pamoja na Taifa Stars.”

 

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro ili kujua ukweli wa taarifa hizo alisema: “Kiukweli nikisema ndiyo au hapana vyote itakuwa ni uongo, ukweli ni kwamba focus yetu ipo kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation na kuwania ubingwa wa ligi," .

 

Msikilize Kessy mwenyewe: “Kusema ukweli mkataba wangu na Mtibwa Sugar unamalizika mwishoni mwa msimu na kwa sasa nipo huru kuongea na timu yoyote, habari za Yanga ni mpya kwangu lakini ikitokea wananihitaji nitakwenda kucheza kwa sababu ni kati ya timu zilizonipa heshima.”

 

Kessy aliwahi kucheza Yanga kwa misimu miwili kuanzia 2016-18, akijiunga na timu hiyo akitokea Simba, kisha 2018 akatimkia Nkana alikocheza kwa misimu miwili, kabla ya kurejea nchini na kusaini kandarasi ya miezi sita kukipiga na Mtibwa Sugar.

1 COMMENTS:

  1. Kama mchezaji na viongozi wamsem hivyo, nuie hizo habar za kutakuw yanga mmezitoa wap

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic