May 19, 2021


 NYOTA wawili wa kikosi cha Kaizer Chiefs wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa robo fainali ya pili unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22. 

Wachezaji hao ni pamoja na kiungo Khama Billiant raia wa Zimbabwe na Dumisani Zuma ambao wanasumbuliwa na majeruhi.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa FNB Soccer Citym ubao kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Uongozi wa Simba uliweka wazi kwamba una mlima mzito wa kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Kikosi cha Kaizer Chiefs kinatarajiwa kutua ndani ya wiki hii ili kufanya maandalizi ya mwisho huku tayari wakiwa wameshatumwa wawakilishi wao Bongo kuandaa mazingira. 

3 COMMENTS:

  1. Na wale watatu wakifika tu bongo watakuwa na korona, so tunawapiga goli 6 kwa 1 kisha tunatinga nusu fainal, tunamliga Al ahyl na kutinga fainal. Na kubeba ubingwa wa afrika.

    ReplyDelete
  2. Hatutaki Fitna wao hawakuwambia mna Corona msiwe wahuni mtafungiwa

    ReplyDelete
  3. Kumguni nyie hakuna cha CORONA wala nn kipigo cha 4G kiendelee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic