WAWAKILISHI wa Tanzania malengo yao ya kutinga hatua ya nusu fainali yamekwama jana Mei 22 Uwanja wa Mkapa baada ya mlima wa mabao 4-0 waliyofungwa nchini Afrika Kusini kuwa ngumu kwao kuupanda.
Licha ya kuishia kufunga mabao 3-0 na kufanya jumla ya mabao kuwa Simba 3-4 Kaizer Chiefs, uongozi wa Simba umewapongeza vijana wao kwa jitihada walizozifanya.
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imekuwa kikwazo kwa Simba ambayo iliweza kuonyesha uwezo mkubwa Uwanja wa Mkapa kukwama kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu fainali.
Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa walipambana kwa hali na mali ila bahati haikuwa yao.
Mabao ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco ambaye alitupia mabao mawili dakika ya 24 na 56 na lile la tatu lilipachikwa na Clatous Chama dakika ya 86.
Kwa sasa Simba na Namungo ambao walikuwa ni wawakilishi wa Tanzania kimataifa wanabaki Tanzania kuendelea kupambana katika Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Juu ya hayo yote Kiwango alichoonesha jana Mnyama kilikuwa kikubwa sijawahi kukiona. Kocha wa Kaizer Haku anacho kile kicheko chake chake cha kukebehi alichoonesha kule kwao na hakuwa mtulivu kiwanjani na wachezaji wake wakawa kama wamepooza Mnyama akiumiliki mchezo kila wakati na kila kona na Simba wameuwaga mchezo lakini kwa sharafu kubwa sana na wala hawatoisahau Simba. Simba jamani Simba.
ReplyDeleteNilikuwa najiuuliza jee hii ndio simba ninayoifaham .. waliwafumika Kaizer Chief katika idara zoote. Nawapongeza sana Simba.
ReplyDeletehongera mtani umejitahidi kusema kweli na ukiendelea kama hivi kuna siku utaushangaza umma wa africa na dunia kwa ujumla mtani jipange upya kwani kufanya vizuri kwa timu yoyote ni kusafisha njia kwa timu zingine kwenye nchi yetu muache anaekucheka maana hajui nini faida ya kufanya vizuri kimataifa
ReplyDeleteHatuna wataalam
ReplyDeleteLisa lilifanyika south africa
ReplyDeleteKosa lilifanyika south africa tupunguze maneno ya mdomoni
ReplyDeleteAlly ahly bingwa
ReplyDeletelabda pia kutokana udogo wa ligi yetu au eti wadau
ReplyDeleteNasikia Ahly wameshangilia sana Mnyama kutolewa kwa sababu ndio timu pekee aliokua amiihofia katika safari yake ya kutetea ubingwa wake
ReplyDelete