KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa, mashabiki wameruhisiwa kuingia ila watafanya maombi mengine ili kuruhusiwa mashabiki wengi zaidi.
Hii inatokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vinaisumbua dunia kwa sasa.
Ni Simba v Kaizer Chiefs unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ule wa awali wakati Simba ikikubali kichapo cha mabao 4-0 hakukuwa na mashabiki ambao waliruhusiwa kuingia katika mchezo huo.
Sasa Mei 22 uongozi wa Simba umesema kuwa umeruhusiwa kuingiza mashabiki ambao wamepata nafasi ya kuingia kwenye mchezo huo.
Haji Manara amesema:"Mpaka sasa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 lakini tunaendelea kuomba kuongeza. Naomba uwanjani rangi iwe nyekundu na nyeupe," .








Kumbe Haji Manara alikusanya tena ile anaitwa Takataka😂😂😂😂
ReplyDeleteHii ni mechi ya Morrison.Kama simba wanataka kuwachanganya Kaiser chiefs mapema basi Morrison lazima aanze mapema.
DeleteOmbeni pi muingie na paka elfu moja wa rangi zote ili mradi ushindi upatikane
ReplyDeleteOmbi langu kwa wachezaji wetu wa Simba ushindi wa goli 5-0 unawezekana lakini lazima wajitoe kufa kupona, acheni mbwembwe za pila biriani, kila mchezaji wa safu ya mbele ya ushambuliaji na hata viungo (7,8,9,10,11) apambane kuingia ndani ya 18 ya Kaizer na hata nje ya 18 na apige mashuti golini kwa Kaizer mara 4 au 5. Kwa wastani huo tunaweza kutegemea kuona majaribio ya maana. Huwezi kupata goli bila kupiga mashuti golini kwa wapinzani wenu. Simba wakiacha kudharau inao uwezo wa kufunga magoli kill dakika 15.
ReplyDeleteMeza ishapinduliwa kibabe, Simba nusu tushaingia anayebisha ahsubiri j'mosi aone wanavyoliwa
ReplyDelete