May 19, 2021


 NAHODHA wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa ikiwa timu yake hiyo ya zamani itashuka daraja na kushiriki Ligi Daraja la Kwanza itakuwa ni aibu.

Jna Mei 15 wakati Mtibwa Sugar ikisepa na pointi tatu mazima mbele ya Tanzania Prisons kwa ushindi wa bao 1-0, Mexime alikuwa Uwanja wa Jamhuri akishuhudia mtanange huo.

Baada ya mchezo kuisha ambapo ulirushwa mubashara na Azam TV alisema:"Sisi wengine Tanzania tumecheza timu moja na tulikusanyana vijana na kusema kwamba tuje, tumekaa na vijana tangu asubuhi na kuwaambia kwamba wafanye utulivu wataokoka.

"Tupo kwenye mwendelezo mzuri na kwenye mechi hii kwa kuwa tumekuja sisi nyingne watakuja wengine, ni kitu ambacho kinaeleweka na  ni kitu kizuri kwa sababu Mtibwa Sugar ikishuka na aibu.

"Kwa mechi tano ambazo zimebaki tunaelewa kwamba Mtibwa ina wachezaji bora na tunajua kwamba ligi ni nguu tuna jukumu la kuwaweka sawa kisaikolojia nina amini kwamba kila kitu kinawezekana," .

Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 na imebakiwa na mechi tano mkononi.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Mbeya City ambayo nayo inapambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa ipo nafasi ya 11 na pointi zake ni 33.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic