DAVID Luiz staa wa Klabu ya Arsenal ametoa taarifa kwamba ataondoka ndani ya timu hiyo msimu huu utakapomeguka.
Luiz alijiunga na Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kipindi cha majira ya joto mwaka 2019 akitokea Chelsea baada ya kukosa nafasi zama za Frank Lampard.
Beki huyo katika msimu wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo alipitia kipindi kigumu kutokana na kufanya makosa ambayo yaliigharimu timu hiyo ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Manchester City.
Licha ya makosa hayo Arteta aliendelea kumuamini na mpaka wakafanikiwa kutwaa Kombe la FA katika kikosi hicho.
Msimu huu hajawa na nafasi ya moja kwa moja ndani ya kikosi cha Arsenal kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Newcastle hivi karibuni.
Taarifa zinaeleza kuwa staa huyo ameomba kuondoka pale mkataba wake utakapoisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment