May 15, 2021


NAMUNGO inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Moroco imegawana pointi mojamoja na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa leo Mei 15.

Licha ya Namungo FC kuanza kwa kasi kipindi cha kwanza jitihada zao ziligonga mwamba kumtungua kipa Metacha Mnata ambaye alitimiza jukumu lake kwa usawa.

Hashim Manyanya na Relliats Lusajo walijaribu kufanya mashambulizi ila walikwama kufunga huku kwa upande wa wageni Yanga kupitia kwa Saido Ntobanzokiza, Zawad Mauya na Yacouba Songne mambo yalikuwa magumu pia kwao.

Kipindi cha pili Yanga waliweza kuwa imara na kufanya mashambulizi kadhaa ila haikuwa bahati kwao kuweza kushinda.

Morocco aliamua kuwaambia vijana wake wajilinde zaidi mbele ya Nassredine Nabi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.

Bao la Yanga walilofunga dakika ya 74 kupitia kwa Yacouba Songne lilifutwa na mwamuzi wa pembeni jambo ambalo lilizua utata kwa wachezaji wa Yanga wakiongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto.

Sare hiyo inawafanya Namungo FC kufikisha jumla ya pointi 36 ikiwa nafasi ya 10 na Yanga inafikisha jumla ya pointi 58 ikiwa nafasi ya pili.

4 COMMENTS:

  1. Wakati umefika tukae na tujifikirie tunakosea wapi kwani tumekuwa kama sikio lisilosikia dawa

    ReplyDelete
  2. Mtoeni Sarpong, mrudisheni Mbili. Pilill mtoeni Fiston mrudisheni Makambo au here Molinga au atakayefaa zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic