May 19, 2021


 WAKATI wadau wengi wa soka wakiamini kuwa ndoto za Simba kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimeyayuka kufuatia kichapo cha mabao 4-0, lakini hali hiyo ni tofauti kwa Kocha Didier Gomes ambaye anaamini kuna maajabu yatatokea kwa Mkapa.

 

Gomes alisema raha ya mpira ni sayansi iliyopo wazi, kwani kama kuna watu waliamini watashinda ugenini au kutoka sare na mwishowe wakafungwa, basi hata kwa Mkapa kuna matokeo yasiyotarajiwa na wengi yanaweza kutokea.

 

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini, Soccer City, Gomes alisema licha ya kupoteza kwa mabao mengi haina maana kuwa walicheza vibaya.


“Tulifungwa siyo kwa sababu hatukucheza vizuri, tulikuwa bora uwanjani na tulifanya kila kitu tulichopanga ila bahati haikuwa kwetu na ile ndiyo tafsiri ya soka, hakuna ambaye anaweza kulitabiri.

 

Hatujatolewa kwenye mashindano kwa sababu bado tuna dakika 90 zingine tukiwa Dar es Salaam, naamini kuna jambo tunaweza kufanya, kwa sababu mpira ni sayansi ambayo ipo wazi,” alisema Gomes.


Baada ya kupoteza mchezo huo wakiwa nyumbani, Simba wanajipanga kwa mchezo wa marudio utakaopigwa Mei 22 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na wanatakiwa kushinda mabao 5-0 ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali.

 


11 COMMENTS:

  1. Simba wanajisumbu. Hawana uwezo wa kuwafunga Kaizer Chiefs 5-0. Sana sana Simba watafungwa 3-0.

    ReplyDelete
  2. Wawe waangalifu tu wakati wa kupindua meza isije ikawafunika wao wenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wiki yenu hii Ila tunajua baada ya muda utasikia wale wachezaji wa kaizer chiefs maduka,Mara Simba mlitumia paka kupindua meza kwa hiyo nyie kwa maneno sisi hatuwawezi taarabu si ndo zenu hatushangai mkaja na sababu lukuki Usimwone Simba kaloa ukadhani paka

      Delete
  3. Hahahaha labda kupindua benchi au sturi ila meza weee thubutu, mtalufa kama 2 bila biashara yenu iishie hapo

    ReplyDelete
  4. It has been revealed by Thato Matuka of Brand Arc, that midfielder Luis Miquissone, whose stint with Downs went very much under the radar, is now their client.

    He shared an image of the two of them in Johannesburg before the player could jet out back to Tanzania with his current club, Simba SC.

    Miquissone had travelled here with his team for their CAF Champions League quarterfinal first leg against Kaizer Chiefs, who thrashed Simba 4-0 on Saturday night.

    ReplyDelete
  5. Luis asaini Kaizer chiefs miaka 4

    ReplyDelete
  6. Manara alisema walicheza hovyo ila mwalimu yeye anasema hawakucheza vibaya du kumbe Manara kweli filimbi

    ReplyDelete
  7. Mikia umwamba wenu umekwisha na msimu huu yanga inachukuwa ubingwa na tutahahakikisha alichoshindwa Simba at akifanya Yanga kwani tutazifunga Al Ahli ya Misri na Kaizer Chiefs nyumbani na ugenini pindi ikiwa tutapangwa nao na hapo ndipo kila mmoja atapofunga mdomo kwa kuinyanyua Yanga wa historia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kufanya hivo ni mpaka mshindeh league na kiufupih ata azam federation hulambii😃

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic