May 26, 2021


 KATIKA kuhakikisha msimu ujao wanafanya vema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes amewaambia mabosi wake kuwa anahitaji wachezaji wanne pekee kutoka nje ya nchi.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo iondolewe na Kaizer Chiefs ya nchini Afrika katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

 

Simba imeondolewa na Kaizer Chiefs baada ya kufungwa jumla ya mabao 4-3 ambapo ugenini ilifungwa 4-0, kabla ya juzi kurejeana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kufanikiwa kupata ushindi wa 3-0.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Gomes ametoa mapendekezo hayo ya usajili baada ya kukutana na mabosi, akitaka beki wa kati, kiungo mchezeshaji, winga na mshambuliaji.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa usajili wa wachezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kutengeneza kikosi chenye ubora kitakachofanya vema katika michuano ya kimataifa baada ya msimhuu kutolewa hatua ya robo fainali.

 

Aliongeza kuwa, jukumu hilo la usajili ameachiwa Gomes atakayefanya kazi pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba chini ya mwenyekiti, Mohamed Dewji ‘Mo’ katika kufanikisha kukisuka kikosi kitakchokuwa imara na tishio zaidi ya msimu huu.


“Msimu ujao tarajia kuiona Simba imara na bora zaidi ya msimu huu ambayo imefika hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa rekodi nzuri ya kutofungwa nyumbani.

 

“Hiyo ni kutokana na mipango ya usajili iliyopangwa na kocha Gomes ambaye tayari amewaambia mabosi wake kuwa anahitaji wachezaji wanne kutoka nje ya nchi wenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kucheza michuano ya kimataifa.

 

“Katika kuhakikisha anakifanyia maboresho kikosi chake, Gomes ametoa mapendekezo yake ya usajili akiomba wachezaji wanne wapya wa kigeni watakaocheza nafasi ya beki, kiungo mchezeshaji, winga na mshambuliaji wenye viwango bora,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Gomes hivi karibuni alizungumzia mipango yake ya usajili na kusema kuwa: “Muda wa usajili bado, hivyo ni vema tukasubiria, hivi sasa akili zetu tumezielekeza katika kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.”

4 COMMENTS:

  1. Nina wasiwasi Kama kweli usajili huo ni wa kocha.Tatizo kuu la Simba ni kipa,kwani Manula anafungwa magoli mepesi mno,wote tumeshuhudia kule South Africa,mipira ya cross haendi.Number nyingine ni upande wa Tshabalala.Viungo na washambuliaji wapo wa kutosha pamoja na walinzi wa Kati wapo sawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui mpira wewe mtoa post, rekodi ya Manura haina poyoyo amekuwa Bora wakati wote, Yale makosa ni ya beki zetu Wala Manula asialaumuwe

      Delete
    2. Yapu nikweli mkuu hujakosea

      Delete
  2. Naungana na mdau wa hapo juu,Mwameja ashawahi kusema Simba imtafute mbadala wa Manula.Zamoyoni Mogella naye alisema ,vilevile hata Jamhuri Kiwelu alisema Manula anafungwa magoli mepesi mno,hivyo inabidi Simba imtafute mbadala wake lakini mpaka leo kimya.Inabidi saa nyingine washabiki tukubali ukweli ili utuponye,Manula anafungwa magoli ya kijinga,South magoli mawili yalikuwa ya kijinga,hivyo ni kweli Simba inahitaji mbadala wake kwa haraka,la cvyo tutamtetea lakini kwenye mashindano ataendelea kutu cost

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic