May 29, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Mei 29 kimesepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo FC.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Namungo 1-3 Simba.

Ni Styve Nsigimasabo alianza kumtungua Aishi Manula dakika ya 21 na kuwafanya Namungo kuutawala mchezo dakika 45 za mwanzo.

Kipindi cha pili Simba ilianza kurudi kambani kwa kupitia Chris Mugalu dakika ya 78, nahodha John Bocco dakika ya 83.

Msumari wa mwisho ulipachikwa na mzee wa kukera Bernard Morrison ambaye alipachika bao hilo akiwa nje ya 18 kwa shuti lililomshinda mlinda mlango, Nahimana Jonathan.

Simba inafikisha pointi 64 ikiwa nafasi ya kwanza Namungo nafasi ya 8 na pointi 40.

13 COMMENTS:

  1. Gongo hodari sana kutoa matamko. Kesho watatoa tamko kwa kuota kuwa ubingwa bado hauna mwenyewe na kuwa msimamo wao ni kukomba makombe yote na katika resi za kugombea kombe la African Championship mwakani yaani baada ya kushikwa mkonio na Simba kuwa watafika mbali kuliko mnyama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani hao "degedege fc" aka utopolo ningependa sana wakose hata nafasi ya pili wanamakelele ya hovyo!

      Delete
  2. Usibishane na kichaa maana wewe ndie utakaeonekana chizi,yanga wanajifariji ila ukweli wanaujua mbona,ngoja aikose hata hiyo nafasi ya pili Kwa laana wanazojizolea kutoka Kwa Simba,haiwezekani mtu akusaidie mpaka unapata mafanikio flani then unamtukana nakumdhihaki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. YAANI WE ACHAS TU, KIFUKWE ANASEMA FAINALI YA FA WAKIKUTANA SIMBA LAZIMA WABEBE NDOO WASEPE NAYO

      Delete
    2. Labda watabeba ndoo ya chooni,Simba ya sasa kufungwa labda kocha aamue tu Ila sio rahisi kama wanavyodhani,mfano wengi walitegemea leo Simba angekula nyasi.

      Delete
  3. jamani simba sio nyau! yaan umkute simba amelala half umshike mkia unajitakia mema kweli!??? tukutane July

    ReplyDelete
  4. dogo ball boy amefurahi kweli nyuma Bocco

    ReplyDelete
  5. They should also know that when Simba exposes his teeth, don't take it for granted that he is smiling with you otherwise he will chop in pieces, exactly what we witnessed yesterday with Namungo who thought the lion had his sharp dangerous teeth choped

    ReplyDelete
  6. When the lion roar who will stand? That is the message for Utopolo before FA Final

    ReplyDelete
  7. Wana Simba wenzangu tumshukuru Mungu coz tumepata ushindi mnono,ila tumtafute mbadala wa Manula maana bado anafungwa magoli ya kipuuzi,Kama goli la Jana kwa level yake hakustahili kufungwa.Ila pamoja na hayo yote Simba ni baba lao,wakubali wakatae hakuna wa kujifananisha na Simba kwa nchi hii,ubingwa in four row unakuja,wakubali wakatae

    ReplyDelete
  8. Wapenzi wa Simba ni Wengi sana na wapo nchi tofauti duniani na Mnyama anapocheza huwepo kwenye media zao na kuishangilia

    ReplyDelete
  9. Unayemlaumu Manula una lako.Hiyo mechi umehadithiwa au vipi?Mpira umemgonga Wawa aliyejaribu kuuzuia na ukageuza mwelekeo Manula angefanya nini?Uliona sevu dhidi ya Dodoma Jiji ?Uliandika kusifia?Au kila goli akifungwa ni kosa lake?Tubadilike.

    ReplyDelete
  10. hivi kesi ya Morrison imeishia wapi?
    haiwezekani akawa anafanya mambo kama yale halafu anaachiwa tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic