MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Simba, leo Mei 26 wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya robo fainali.
John Bocco alipachika mabao mawili dakika ya 22 na 41 na kuwafanya Simba kwenda mapumziko ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.
Kipindi cha pili, Dodoma Jiji waliongeza jitihada kusaka bao la ushindi ila walikwama kupenya ngome ya Pascal Wawa na Kened Juma ambao walikuwa wakicheza kwa maelewano.
Bao la tatu lilipachikwa na Meddie Kagere ambaye anafikisha jumla ya mabao matatu ndani ya Kombe la Shirikisho.
Ushindi huo unaifanya Simba kutinga hatua ya nusu fainali na itakutana na Azam FC ambayo imeshinda leo mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.








Kipindi cha pili dodoma jiji waliongeza jitihada kusaka bao laushindi!! Anyway nusu fainali lini na wapi??
ReplyDeleteNa wakalipata kupitia kwa mk 14
DeleteBao la ushindi au bao lakufutia machozi?ndugu vp?unamilik smartphone alafu unayoyafanya hayaendani why????
ReplyDeleteDodoma jiji wanadai mmepuliza dawa,jee ni kweli??,thibitisheni kama sio ukweli
ReplyDeleteDawa gani hiyo iliyopulizuwa, kwani hawakujuwa kuwa walikuwa wakicheza na bingwa aitwae Simbaaa? Na hapohapo Mnyama ndio anapiga hodi matopeni fungeni milango tena muingie mitini
ReplyDeleteWamepuliza dawa ya kuua wadudu au?debe tupu haliachi kuvuma ni kawaida yenu kila akishinda Simba lazima mtie figisu,mungu awabiriki na mtavuna mlichokipanda.
ReplyDelete