May 17, 2021


 WAKATI Yanga Mei 15 ikilazimishwa suluhu na Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, gumzo kubwa ni kukataliwa kwa bao la Yanga lililofungwa na Yacouba Songne dakika ya 73 kwa kona iliyochongwa na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.

 

Yacouba ambaye aliukwamisha mpira huo kimiani kwa kichwa akiunganishiwa pasi ya kichwa kutoka kwa Tuisila Kisinda, lakini bao hilo lilikataliwa kwa tafsiri kwamba mpira ulitoka nje kabla ya mfungaji hajafunga bao hilo.

 

Kukataliwa kwa bao hilo, kukawafanya wachezaji wa Yanga, kumzonga mwamuzi wa pembeni ambaye aliokolewa na mwamuzi wa kati, Hans Mabena.

 

Mwamuzi mstaafu aliyekuwa akichezesha mechi za Ligi Kuu Bara, Othman Kazi, amemaliza utata huo kwa kuliambia Spoti Xtra kwamba: “Kabla ya mpira kumfikia Yacouba, mpira ulikuwa umetoka nje na kurudi uwanjani, hivyo haliwezi kuwa bao halali ndiyo maana mwamuzi wa pembeni alinyoosha kibendera juu kabla hata bao halijafungwa kuashiria kwamba kuna makosa yamefanyika," .


HALI YA MCHEZO


Katika mchezo huo, licha ya jitihada za nyota watatu walioanza kikosi cha kwanza ndani ya Yanga ambao ni Kisinda, Michael Sarpong na Saido, hakuna ambaye aliona lango la mpinzani wake.

 

Namungo wataijutia nafasi ya wazi ambayo waliikosa kupitia kwa Hashim Manyanya dakika ya 8 ambaye alikuwa ndani ya 18, akapiga shuti lililokwenda nje kidogo ya lango la Yanga, huku Yacouba naye ataikumbuka nafasi aliyokosa dakika ya 66 baada ya kipa Jonathan Nahimana kuokoa hatari.


Saido alipiga jumla ya pasi 22, alikokota mpira mara tano huku akipiga jumla ya faulo tatu na kona 7.

 

Sarpong alitumia jumla ya dakika 62 na nafasi yake ilichukuliwa na Ditram Nchimbi ambapo alipiga jumla ya pasi 21, mashuti yaliyolenga lango yalikuwa mawili na mawili hayakulenga, huku akichezewa faulo nne.


Kisinda spidi zake zilikuwa zikipambana na Jafary Mohamed, alipiga pasi 33, alikuwa kwenye ubora wake licha ya Uwanja wa Majaliwa kuwa na changamoto kutokana na ubora kuwa mdogo sehemu ya kuchezea.

 

Suluhu hiyo imezidi kufifisha matumaini ya Yanga kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo sasa imefikisha pointi 58 ikiwa pointi tatu nyuma ya vinara Simba wenye 61.Yanga mpaka sasa imecheza mechi 28, imebakiwa na mechi sita kukamilisha msimu huu, huku Simba ikicheza mechi 25, ina mechi tisa mkononi kuhitimisha msimu.

 

Katika mechi tisa ilizobaki nazo Simba, inahitaji ushindi wa mechi tano tu ili kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo itakuwa imefikisha pointi 76. 


Kumbuka katika mechi hizo, miongoni mwao itakuwa ni ile dhidi ya Yanga.Yanga ikiwa imebakiwa na mechi sita, ikishinda zote itamaliza msimu na pointi 76.

14 COMMENTS:

  1. Kwa ninavowajuwa Yanga si hasha wakakimbilia Fifa kulidai goli

    ReplyDelete
  2. Acha tusubiri,kwani muda utafika na tutaona tusiyoyatarajia.

    ReplyDelete
  3. Nyamazeni, nyie mmpigwa nneee,kama vile wamesimama

    ReplyDelete
  4. Ndio mana mkaukosa ubingwa kwa muda wa miaka mine mfululizo. Watapokuha Kaizer hebu ombeni mechi ya kirafiki nao ili kuwaonesha Simba kuwa mnastahili ubingwa

    ReplyDelete
  5. Othman Kazi siyo mchambuzi Mzuri yupo bias sana. Ni mnyama OG.

    ReplyDelete
  6. Ahahah Othman Kazi amejuaje kama mpira ulitoka? Wakati anaangalia kwenye Tc kama wengi waivyoona, au ndio mchambuzi mnazi wa Simba, au ndio waleo wanaoitwa Takataka na msemaji wao?

    ReplyDelete
  7. Mwambie aache uongo lile ni hili ila Kwa mapenzi yake amelikataa sawa tu yeye si ndio muamuzi ila na sisi tumekubali ila atutaki visababu

    ReplyDelete
  8. Kilichpmwachisha kazi ya uamuzi si alikamatwa kwa Rushwa Songea. Sasa anaeleza nini

    ReplyDelete
  9. Huyu Othman Kazi ni kiazi....nani asiyemjua kuwa yeye ni shabiki wa Vimburu,alipigwa chini kwa sababu ya kuchukua rushwa na pia baada ya kuwa dalali wa mikia kwa kuwafikishia hongo marefa.Asitake tumvue nguo zaidi

    ReplyDelete
  10. Hilo goli mbona haulizwi aliyelikataa akatoa sababu za kulikataa,cha ajabu mnamsemea!,hizi ni mbinu potofu za kuiangusha Yanga,hui ndiyo ukweli,upo,ujanja ujanja tu mnafanya.

    ReplyDelete
  11. Fungeni magoli yaso na utata, mnataka kila siku kila jambo liwe upande wenu wazee inawezekanaje?

    ReplyDelete
  12. Sisi tumepigwa nne na wewe tumekupiga 4 mara nyingi kwa hiyo sishangai hilo maana nacheza na timu kubwa Africa siyo Tanzania

    ReplyDelete
  13. Yule Refa alijilipua makusudi ili kutupoteza hao paka hawachezi Ligi wanasikilizia matokeo ya Yanga na wanaingilia waamuzi wanavuruga maksudi akijua atafungiwa mechi tatu huku kapokea milioni kumi mbwa tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic