BAADA ya kumalizana na Namungo FC kwenye sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa kwa sasa hesabu za Yanga ni mbele ya JKT Tanzania.
Mchezo wao dhidi ya Namungo ilikuwa ni Mei 15 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Namungo 0-0 Yanga jambo lililowafanya wagawane pointi mojamoja.
Kituo chao kinachofuata ni dhidi ya JKT Tanzania, Mei 19 Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ngoma ilikamilika Yanga 1-0 JKT Tanzania hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.
Nahodha msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ili kufikia malengo waliyojiwekea.
"Bado tuna kazi ya kufanya na kwa sasa akili zetu ni kwenye mechi ambazo zinafuata na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri," .
Bila ya shaka ubingwa mtaupata na atayehakikisha ubingwa huo ni wewe mwenyewe, kwa hivo zidi kuchemka usiwe unaikosakosa namba yako
ReplyDelete