May 2, 2021


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa aliamua kufanya mabadiliko kwenye mchezo wao wa jana wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar ili waongeze nguvu ya kumiliki mchezo jambo ambalo alifanikiwa kulifanya. 

Ameongeza kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga wanahitaji kupata ushindi kwa sababu ikiwa wakishinda mchezo huo wa ligi watakuwa mabingwa.

 Pia ameweka wazi kwamba mchezaji wake Bernard Morrison ambaye aliingia akitokea benchi ni miongoni mwa wachezaji ambao wanafanya vizuri na hana uhakika kama anaweza kuanza mbele ya Yanga, Mei 8 ila ni suala la kusubiri. Katika mchezo wa jana Simba ilishinda mabao 2-1 ambapo ni Morrison alifunga bao moja na alitoa pasi moja kwa Meddie Kagere na lile la Kagera Sugar lilifungwa na Eric Mwaijage.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic