KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi anatarajiwa kuwakosa nyota wake sita leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Wachezaji hao sita wamehusika katika jumla ya mabao 10 kati ya 41 ambayo yamefungwa na kikosi hicho baada ya kucheza jumla ya mechi 28 na pointi zake ni 58.
Nyota hao ni pamoja na Abdalah Shaibu, ‘Ninja’, Yassin Mustapha, Mapinduzi Balama na Carlos Carlinhos mwenye mabao matatu na pasi mbili za mabao kiungo Haruna Niyonzima huyu ana matatizo ya kifamilia.
Pia beki kisiki Lamine Moro huyu kosa lake la utomvu wa nidhamu lililomfanya aondolewe kikosini Mei 15 litamfanya awakose JKT Tanzania.
Lamine yeye amefunga jumla ya mabao manne na ametoa pasi moja ya bao kati ya mabao 41 ambayo yamefungwa amehusika katika mabao matano.
Ni Mwinyi Kazimoto kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Mohamed Abdalah, ‘Bares’ kwa upande wa JKT Tanzania atakosekana kwa kuwa bado hajawa fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alipotafutwa na Spoti Xtra ili azungumzie hali ya wachezaji hao alieleza kuwa yupo kwenye kikao.
0 COMMENTS:
Post a Comment