May 19, 2021


 NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Prince Dube amezidi kuutikisa ufalme wa kucheka na nyavu uliopo mikononi mwa Meddie Kagere.

Kwa sasa ikiwa ni mzunguko wa pili na Azam FC imecheza jumla ya mechi 29 na kutupia mabao 42, yeye amehusika kwenye mabao 18 akifunga mabao 13 na kutoa pasi tano za mabao jambo ambalo halijafikiwa na mshindani wake namba moja Kagere.

Simba ikiwa imecheza mechi 25 na kutupia mabao 58, Kagere amehusika kwenye mabao 11 ambayo ameyafunga na kwenye msimamo wa utupiaji yupo nafasi ya pili.

Kagere anatetea kiatu chake cha ufungaji alichokitwaa msimu uliopita baada ya kufunga mabao 22 na pia msimu wa 2018/19 alitupia mabao 23 hivyo ana kazi ya kufanya kufikia malengo yake.

Dube kuhusu kiatu cha ufungaji alisema:"Ninapenda kufunga kwa kuwa ni jukumu langu hivyo nitazidi kupambana,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic