May 15, 2021


WAKATI leo Mei 15 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kikitarajiwa kusaka ushindi mbele ya Kaizer Chiefs majira ya saa 1:00 usiku kuna nyota saba wanaweza kuukosa mchezo wa leo.

Tayari Simba ipo Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Miongoni mwa nyota ambao wanaweza kuukosa mchezo wa leo ni pamoja na Ally Salim kipa namba tatu wa Simba, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael bado hawajawa fiti kwa ajili ya mchezo wa leo.

 John Bocco ambaye ni nahodha wa Simba imeelezwa kuwa ana asilimia 50 kuanza ama kutokuanza kwa kuwa bado hajawa fiti. 

Miraj Athuman na Said Ndemla hawa wameachwa Bongo kutokana na sababu mbalimbali huku Perfect Chikwende yeye hajasajiliwa kwa mashindano ya kimataifa yupo kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Meneja wa Simba, Patrcik Rweyemamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na watapambana kupata matokeo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic