May 30, 2021


 BAADA ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kutangaza kuachana na straika Mzambia, Lazarous Kambole itakuwa ni njia rahisi kwa mabosi wa Jangwani, Yanga kuipata saini yake.

 

Katika msimu uliopita, Yanga ilikuwepo katika mipango ya kumsajili Mzambia huyo kabla Chiefs kuingilia kati na kumnasa kwa dau la dola 200,000 (zaidi ya Sh 459m) akitokea Zesco United.

 

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chake ikiwemo safu ya ushambuliaji ambayo imeshindwa kuonyesha makali inayoongozwa na Mghana Michael Sarpong na Fiston Abdoulrazack.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi, kutoka Chiefs upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kuachwa katika mipango ya klabu hiyo baada ya kufanya vibaya katika ligi.

 

Chiefs itaachana na nyota huyo kwa lengo la kuacha nafasi ya kumsajili mshambuliaji mwingine mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao zaidi ya Kambole ambaye hana nafasi ya kudumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

 

Klabu hiyo iliyofuzu Hatua ya Robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwaondoa Simba kwa kuwafunga mabao 4-3.

 

Yanga ina nafasi kumnasa mshambuliaji huyo kutokana na mahusiano mazuri yaliyokuwepo hivi sasa mdhamini wa klabu hiyo, Kampuni ya GSM.

 

Yanga kwa kupitia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alitembelea Klabu ya Chiefs kwa ajili ya kujenga uhusiano kati ya klabu hizo mbili.

 

Yanga kwa kupitia Mshauri wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa, hivi karibuni alisema: “Uongozi umepanga kufanya vitu vyake kwa usiri mkubwa tofauti na misimu miwili iliyopita, lengo ni kufanya usajili utakaokuwa bora na kisasa.”

5 COMMENTS:

  1. UNAWEZA KUFANYA SIRI LAKINI USIFANYE USAJILI BORA, YANGA ACHENI UKAKASI NA UJANJA UJANJA KATIKA KUENDESHA TIMU. MLISEMA FISTON MTAMBO WA MABAO, LEO YUKO WAPI? SARPONG? YACOUBA? NA WENZAO WOOTE! MMEMCHUKUA SENZO KAMA MSHAURI JE MMEHARIBU KILA KITU KWA USHAURI WA SENZO?...................YAJAYO YANAFURAHISHA, MOJAWAPO NI SIMBA KUTWAA UBINGWA WA 5 MAANA HUU USHACHUKULIWA BADO KUTANGAZWA TU

    ReplyDelete
  2. Kila anayecheza na simba anakuwa na mahusiano mazuri na yanga, vita, mazembe, chiefs. Nini kilicho nyuma ya haya mahusiano?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna mahusiano bali ni kupigwa pesa,na ndiomana wanauziwa magarasa mwisho wa siku kuishia kudanganywa na viongozi wao,LALIGA wanapiga mpunga tu la maana hakuna,mshauri wa mambo ya soka,kwanini msingewekeza kwa washauri wa ndani ya bara la Afrika mbona wamejaa tele na uwezo mkubwa mnoo,yanga isipokua makini itaanguka na chanzo ni uongozi dhaifu,ndani ya uongozi kuna wapigaji wengi sana.

      Delete
  3. Simba bingwa wa vpl na asfc,na watasubiri sana ubingwa wao walishachukua kule Zanzibar.

    ReplyDelete
  4. Yanga acheni kusajili nje hapa ndani kuna wachezaji wazuri tu. Mfano Dickson Amundo anafaa sana kuchukua nafasi ya Cotinyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic