May 12, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi leo Mei 12 kimewasili salama Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Yanga wametua Mtwara na ndege ya Kampuni ya Precision Air ili kuanza kuwavutia kasi Namungo wanaonolewa na Hemed Morroco. 

Ni Mei 15 wanatarajiwa kukutana katika Uwanja wa Majaliwa ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 1-1 Namungo.

Miongoni mwa waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Wazir Junior, Farouk Shikalo na Metacha Mnata.


2 COMMENTS:

  1. Wandishi wa hii blog ni darasa la 7 failures

    ReplyDelete
  2. Labda ni ajabu wao kupanda ndege mabingwa wametuwa africa kusini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic