VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara leo Juni 18 dhidi ya Gwambina FC.
Katika mchezo wao uliopita walipokutana Uwanja wa Gwambina Complex ubao ulisoma Gwambina 0-0 Azam FC.
Bahati amesema:"Tuko vizuri na hakuna mchezaji hata mmoja ambaye tunaweza tukasema kwamba anaweza kukosa.
"Kitu ambacho tunaelewa kwamba mtu ambaye yupo chini mara nyingi anakuwa hana presha ila atapambana kupata matokeo.
"Hilo tunajua ila nasi tunataka kupambana ili kuonyesha kwamba tunaweza kikubwa ni kwamba tunahitaji pointi tatu muhimu," amesema.
Kwenye msimamo, Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi zake ni 60 inakutana na Gwambina iliyo nafasi ya 17 na pointi 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment