June 6, 2021


 KIKOSI cha Azam FC usiku wa kuamkia leo  kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka ushindi, Juni 5.

Ni Mpianza Monzinzi mshambuliaji wa Azam FC alianza kucheka na nyavu dakika ya 21 ambapo alipachika bao hilo kwa kichwa akitumia krosi ya Emmanuel Charles.

Dakika 45 zilikamilika huku ubao ukisoma Azam FC 1-0 Coastal Union na mabao mengine mawili yalipachikwa kipindi cha pili.

Ilikuwa dakika ya 85 ambapo Obrey Chirwa alifunga bao la pili lililojaa kambani na kuwainua mashabiki wa Azam FC.

Bao la tatu lilipachikwa dakika ya 90+2  lilipachikwa na Ismail kwa pasi ya Chirwa na kuwafanya Azam FC wasepe na ushindi kwenye mchezo huo wa kirafiki.

2 COMMENTS:

  1. UNACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA COASTAL UNION UNATAKA UIKABILI SIMBA AMBAYO IMECHEZA MECHI 4 IKIFUNGA MAGOLI 12 NA KRUHUSU GOLI MOJA. VIONGOZI AZAM HAWAKO SERIOUS

    ReplyDelete
  2. Azam imecheza na supa timu yenye kiwango inayoshiriki ligi kuu mojaapo iliyowafunga matopolo ambapo hao matopolo wenyewe hutafuta vitimu visivojulikana eti kujitayarisha kucheza na mnyama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic