June 9, 2021

 


IMEELEZWA kuwa nyoa wa kikosi cha Ruvu Shooting, Edward Manyama amemalizana na mabosi wa Simba kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Nyota huyo ambaye amecheza Ruvu Shooting,  Namungo kwa sasa yupo ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

Habari zinaeleza kuwa ushindani mkubwa wa kusaka saini ya beki huyo ilikuwa kati ya Yanga na Simba ambao wote ni vigogo wa Kariakoo.

Yanga walianza kumfuatilia nyota huyo msimu uliopita alipokuwa ndani ya Namungo dili lake likabuma akaibukia ndani ya Ruvu Shooting.

Alipotafutwa Manyama azungumzie suala hilo alisema kuwa hajui jambo lolote.

3 COMMENTS:

  1. Karibu Sana Msimbazi ila Nina wasiwasi Kama ataweza kumuweka bench Tshabalala

    ReplyDelete
  2. Ni muhimu sana Tshabalala apate changamoto asibweteke

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic