BEN White, beki anayecheza ndani ya kikosi cha Brighton anatajwa kuingia kwenye anga za Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kwa ajili ya kumsajili.
Kwa Arsenal kuhitaji saini yake inaingia kwenye vita na mabosi wa Manchester United, Liverpool na Chelsea ambao nao wanatajwa pia kumtazama kwa ukaribu beki huyo.
Nyota huyo amekuwa bora kwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu England akiwa amecheza jumla ya mechi 36 jambo ambalo limefanya ajumuishwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England chenye jumla ya nyota 26 kwa ajili ya mashindano ya Euro akichukua nafasi ya Trent Alexander-Arnold ambaye anasumbuliwa na majeraha.
Kwa mujibu wa The Mirror imeripoti kwamba Arteta anamkubali beki huyo na atafanya mpango wa kumvuta ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.
Nyota huyo mwenye miaka 23 dau lake linatajwa kuwa pauni milioni 50. Kikubwa ambacho Arsenal kwa sasa wanakitaka ni kuboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment