IMEELEZWA kuwa staa wa Real Madrid, Karim Benzema amekuwa akimshawishi nyota wa PSG, Kylian Mbappe kujiunga na Real Madrid.
Benzema na Mbappe kwa sasa wapo pamoja katika timu ya taifa ya Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Euro na wameonekana wakiwa na ukaribu mkubwa.
Tangu msimu uliopita mpaka sasa kuelekea msimu ujao Real Madrid wanatajwa kuwa na lengo la kumsajili Mbappe.
Nyota huyo bado hajaongeza mkataba wake ndani ya kikosi hicho cha PSG ingawa alianza mazungumzo nao.
Benzema amesema:"Kama (Mbappe) anataka kuondoka, basi aje haraka Real Madrid,".
0 COMMENTS:
Post a Comment