June 7, 2021


WAKATI leo Jumatatu hukumu yake ikitarajiwa kutoka kutokana na kile kilichoelezwa kuwa utovu wa nidhamu, mchambuzi wa masuala ya michezo na nyota wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amesema kuwa huenda mabosi hao wanamtafutia sababu.

Hii inakuwa ni mara ya pili ndani ya msimu wa 2020/21 kwa nyota huyo kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu ambapo zama za Sven Vandenbroeck alisimamishwa na kukosa jumla ya mechi 10.

Kwa sasa zama za Didier Gomes, pia amesimamishwa na mchezo wake wa mwisho kucheza ilikuwa dhidi ya Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini.

Kiemba amesema:"Tangu nacheza nae Mkude ni yule yule na hatukuwahi kusikia haya tunayosikia sasa wala hizi kesi tunazozisikia hivi sasa.

"Nahisi labda kwakuwa haitajiki tena ndani ya timu ndio maana haya tunasikia sana, yanatokea mengi ili siku akiondoka basi Mashabiki wasihoji sana, hii ni sawa na kumpa Mbwa jina baya ili umpige" .

7 COMMENTS:

  1. Kiemba......Zama zinabadilika...zama zinapita na kwenda zake,usilinganishe zama ambazo wewe ulikuwa nae kwenye timu miaka nane iliyopita na zama za sasa ambapo upo nje ya timu lakini Mkude bado yupo kwenye kikosi.Jiulize kwa nini awe yeye tu na si wengine?Hebu jaribu kutafakari hapo.
    Kwa nini isiwe huenda yeye ndo atakuwa amechoka na anafanya vituko ili aondoke?Mkude wa enzi za akina Kiemba ni tofauti na Mkude wa enzi za akina Manula

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anajitafutia sababu na sio anatafutiwa sababu Simba na Taifa stars nako nani anamtafutia sababu?

      Delete
    2. Mnakwenda ugenini kucheza wewe sanabu ni maarufu inaletewa bangi kambini unawapa na wenzio wasiovuta wamekusemea

      Delete
    3. Mnakwenda ugenini kucheza wewe sanabu ni maarufu inaletewa bangi kambini unawapa na wenzio wasiovuta wamekusemea

      Delete
  2. Halafu mwandishi balance habari. Unawasomaji wengi. Swala la mkude unataka kutuambia huna ufahamu nalo! Vinginevyo umeingia kwenye mtego wa kuandika porojo za Kiemba. Sijui hata kaanza lini kuchambua mpira kama huo ndo ucham uzi.

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo kiemba anataka kutuambia kuwa kwa kuwa Mkude ni mtovu wa nidhamu tangu zamani basi viongozi wa Simba waendelee kumuacha tu... Kumbuka Simba ya sasa co ile kwa sasa nidhamu kwanza ndo tunaangalia uwezo wako uwanjani

    ReplyDelete
  4. Kwa nini wasiwe wengine? Sababu ameshapatikana mwingine, atafuata mshambuliaji. Tusubiri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic