KLABU ya Chelsea imeanza mazungumzo na Klabu ya Borussia Dortumund kwa ajili ya kumpata Erling Baraut Haaland licha ya kwamba kuna mazingira magumu ya kuweza kufanikisha dili hilo.
Borussia Dortmund wameweka wazi kwamba hawana nia ya kumuuza mshambuliaji huyo msimu huu ila matamanio ya Haaland ni kuona kwamba timu hiyo inafanya mazungumzo na baadhi ya timu ili kuweza kuona namna gani anaweza kupata changamoto mpya.
Ikiwa dili lake litakamilika dau ambalo linatajwa kumuondoa ndani ya kikosi hicho mpaka kwa Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao ni Chelsea wanaonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel litawagharimu Euro milioni 170.
Chelsea ina wachezaji ambao itahitaji kuwatumia ili kupunguza gharama ya dau hilo ikiwa ni pamoja na Tammy Abraham ambaye dau lake ni Euro 40. Pia Tuchel amemwambia mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kwamba ikiwa atampata mshambuliaji huyo itakuwa faida kwao na wataweza kushindana na timu kama Manchester City ambao nao pia wanatajwa kuwania saini ya nyota huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment