MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Klabu ya Simba kwa sasa ni RUKSA kuzungumza na mabosi wa watani zao wa jadi Yanga ili waweze kupata saini yake.
Nyota huyo mwenye mabao 11 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 dili lake linameguka msimu utakapoisha hivyo kanuni zinampa Tulsa kuzungumza na timu ambayo inamtaka.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba amesema kuwa mteja wake mkataba wake utafika ukingoni ligi itakapoisha.
Yaani nyie waandishi wa hii blog mmeona Yanga ndo China ya Tanzania kwa watu kuja kumalizia mpira wao...
ReplyDeleteHuku ni kuikashifu yanga mwandishi huyu hajui weledi wa taaluma yake
ReplyDeleteNashangaa kwani Yanga umeskia wana shida nae au
ReplyDeleteMchukuweni lakini mumtunze, kumheshimu apewe dau lake na malipo asicheleweshiwe na kiwe kiwango kile alichokuwa akikipata kutoka Simba na kosa lolote la kimpira isiwe anazomewa kama enzi zake katika Simba
ReplyDelete