WINGA wa Bayern Munich, Kingsley Coman amekataa kuongeza mkataba mpya ndani ya kikosi hicho akiwa na nia ya kucheza Premier League.
Dili lake winga huyo linatarajiwa kumalizika Juni 2023 na mabosi wa timu hiyo wanataka kumuongezea dili jipya.
Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Manchester City katika kipindi hiki cha usajili jambo ambalo linamfanya aamini kwamba atakwenda kucheza huko.
Rais wa timu hiyo, Uli Hoeness amesema:"Kwa sasa ni kama tumetulia kwanza kutokana na masuala ya kiuchumi. Kuhusu Coman kama hatakubali kuongeza mkataba mpya basi anatakiwa kupambania kiwango chake," .
0 COMMENTS:
Post a Comment