June 18, 2021


MABOSI wa Tottenham wameamua kumshawishi Gennaro Gattuso aliyekuwa anaifundisha Fiorentina ili awe mbadala wa Jose Mourinho ambaye alifutwa kazi ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo mbovu.

Timu hiyo imeshtua baada ya awali kuhitaji kumpa dili kocha wa zamani wa Roma, Paulo Fonseca ila dakika za mwisho imeelezwa kuwa wamefungua mazungumzo na Gattuso ambaye anahitaji kusepa katika timu hiyo aliyotumikia kwa muda wa siku 23 akiwa ni kocha mkuu.

Licha ya kwamba Tottenham inataka kumpa dili Gattuso tayari Fonseca alikuwa tayari kujiunga na timu hiyo ambapo walianza mazungumzo na kiongozi wa masuala ya michezo ndani ya timu hiyo, Fabio Paratic kuhusu mpango wake wa kuwa kocha ndani ya kikosi hicho.

Spurs wamesisitiza kwamba suala la fedha halihusiani katika mpango wao wa kubadilisha maamuzi na wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya mikakati mikubwa ya timu hiyo. 


 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic