June 7, 2021


 DOZI ambayo kwa sasa Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa wapinzani wao inatoa wanapokutana uwanjani ni mwendo wa tatutatu katika mechi zao ikiwa ni rekodi ya kipekee kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Bongo.


Kazi ilianza Mei 22, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali, ubao ulisoma Simba 3-0 Kaizer Chiefs, ila licha ya ushindi huo ilitolewa kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa FNB  Soccer City ubao ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.


Mei 26, mchezo wa Kombe la Shirikisho mbele ya Dodoma Jiji, ubao ulisoma Simba 3-1 Dodoma Jiji na ushindi huo uliwapa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali.


Mei 29, Uwanja wa Majaliwa, mchezo wa ligi walisepa na pointi tatu mazima na ubao ulisoma Namungo 1-3 Simba funga kazi ilikuwa juzi, Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba ambapo ubao ulisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba.


Katika mechi nne ambazo ni dakika 360, Gomes ameshuhudia jumla ya mabao 12 wachezaji wake wakifunga na kipa wake namba moja Aishi Manula ameokota mabao mawili, kwenye msako wa pointi tisa wamesepa nazo zote wakiwa ni vinara katika ligi na pointi zao 64.

Gomes amesema kuwa kikubwa anachotazama ni ushindi kwenye mechi zao ambazo wanacheza ili kufikia malengo yao.

"Kikubwa ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu na kila kitu kinawezekana kwa kuwa wachezaji wanajiamini na wana uwezo mkubwa," amesema.

 

3 COMMENTS:

  1. Thanks And Regsrds Mr Gomes for your team's tremendous achievements followed by achievements and wish you a very prosperous future

    ReplyDelete
  2. Kwy ASFC Simba na DodomaFC matokeo yalikuwa 3-0, sio 3-1. Mechi ya ligi ya mwisho kati ya timu hizo matokeo ndio yalikuwa 3-1.Kuweni makini.

    ReplyDelete
  3. Simba ina point 67 siyo 64. Kuweni makoni wandishi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic