June 4, 2021


NYOTA wa kikosi cha Simba, Gadiel Michael nafasi yake ya kubaki katika kikosi hicho kwa sasa ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.

Habari zimeeleza kuwa nyota huyo ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea Yanga hana nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo linafanya maisha yake kuwa tofauti na zama zile alipokuwa ndani ya Yanga.

"Nafasi kwa Gadiel inazidi kuwa finyu kikosi cha kwanza jambo ambalo linafanya ashindwe kuanza kikosi cha kwanza na wakati mwingine hata benchi amekuwa akikosekana.

"Jambo jingine ni ushindani wa namba kwa sasa ndani ya Simba ni mkubwa hivyo kuanza kwake na kubaki kwake msimu ujao inategemea maamuzi ya mwalimu mwenyewe," ilieleza taarifa hiyo.

Gomes hivi karibuni aliweka wazi kwamba yule ambaye anaanza kikosi cha kwanza ni mchezaji ambaye atafanya vizuri mazoezini kwa kuwa kuna wachezaji wengi wenye ubora ndani ya Simba.

Baada ya kumalizana na Ruvu Shooting, Mwanza jana Juni 3, leo Juni 4 kikosi kimerejea Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic