June 4, 2021


 KIKOSI cha Yanga kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi imetinga hatua ya nusu fainali ambapo itacheza na Biashara United katika mchezo wa nusu fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Iwapo watashinda mchezo huo watakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali kati ya Azam FC v Simba katika fainali.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Simba inayonolewa a Kocha Mkuu, Didier Gomes. Yanga kupitia kwa Ofisa Habari, Hassan Bumbuli wameweka wazi kwamba wanahitaji kusepa na taji hilo.

Pia mchezo wao wa kirafiki ambao ulitarajiwa kuchezwa Juni 6, saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex umeghairishwa kwa kile ambacho wameeleza kwamba ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Kutokana na kughairishwa mchezo huo Klabu ya Yanga imeomba radhi kwa wanachama, wapenzi na wadau wengine wote ambao wataathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na kufutwa kwa mchezo huo.

5 COMMENTS:

  1. Hahahaaa mganga baada ya ramli kawakataza

    ReplyDelete
  2. Mechi za kirafiki ni muhimu sana lakini.....Kuzikosa mzunguko wa pili ndio zilitu cost

    ReplyDelete
  3. Sababu zilizo nje ya uwezo zipo kwenu tu!, Wakifanya hivyo wenzenu inakuwa nongwa. Sipati picha ingekuwa TFF ndio wameamua mechi kuahirishwa Hilo povu lake lingekuwaje??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulikuwa umeshakata tiketi ndugu? au ulikuwa uwanjani Chamazi?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic