June 4, 2021


 IMEELEZWA kuwa viungo raia wa DR Congo, 
Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ndiyo wamefanikisha usajili wa beki wa AS Vita, Shaaban Djuma.

Tetesi za usajili zinasema kuwa beki huyo tayari amekamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Beki huyo raia wa Congo, atajiunga na Yanga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa kuendelea kukipiga Vita kumalizika, hivyo anaruhusiwa kujiunga na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, beki huyo tayari amesaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa usajili wa beki huyo umefanikishwa na Wacongo wenzake Tonombe na Kisinda ambao ndio walitumia nguvu nyingi kumshawishi nyota huyo kusaini Yanga.

Aliongeza kuwa beki huyo anatarajiwa kujiunga na Yanga mapema mwanzoni mwa Julai, mwaka huu tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

“Kama unakumbuka vizuri, Simba ndiyo walikuwa wakimfuata Djuma kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia muafaka mzuri ya yeye kusaini mkataba.

“Wakati Simba wakipambania kuwania saini ya beki huyo, ndiyo viongozi wa Yanga waliwatumia baadhi ya viongozi wa AS Vita kwa ajili ya kumshawishi asaini Yanga.

“Tofauti na viongozi pia wachezaji wa Yanga, Wacongo wenzake ambao ni Kisinda na Mukoko walishiriki kwa asilimia kubwa kumshawishi ili ajiunge na Yanga, hivyo akakubali na kusaini kwa siri miaka miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mshauri wa Yanga, raia wa Afrika Kusini, Senzo

Mazingisa, hivi karibuni alisema: “Tayari

tumekamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji

na katika hili la usajili, tumekuwa tukifanya kwa

usiri mkubwa.

“Kikubwa hatutaki kuingiliana katika usajili na

timu pinzani kwa kuhakikisha tunawasajili

wachezaji wote walio kwenye mipango yetu.”

8 COMMENTS:

  1. AS Vita wamekubali kuwa tawi la utopolo, kwa maana nyingine ndio itopolo ya Congo

    ReplyDelete
  2. Mchezaji huru wakati mchezaji bado anamkataba. Yanga imara na Simba imara ndipo tunapohitaji hapo. Sio Yanga nyanya halafu wanatumia nguvu kubwa kujilinganisha na Simba imara kwa kutegemea nguvu za Giza.

    ReplyDelete
  3. Hivi ninyi Simba mnashida gani,au kwa kuwa mlizaliwa na shida mkipata mnahisi watu hawakuwahi kupata.

    ReplyDelete
  4. Yani washabiki wa simba cjui niwaitejetu kwanini mfatilie maisha ya mwenzio?ushabiki umeingiriwa kweri yanapwayuka tu!

    ReplyDelete
  5. Tatizo la washabiki wa mikia, hawawezi kuishi bila kutaja Yanga, hawa watu wanA matatizo waliyorisishwa na msemaji wao, zamani hakukua na waropokaji wa aina hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ivi kati ya simba na yanga wapi kuna washabiki maandazi?unapaswa uhoji kwanini muangola mliempokea kama mfalme leo hii amekimbia timu?alafu msemaji wenu anafunguka mubashara kwamba kalinyo hakua na furaha ndani ya yanga isipokua walikua wanatumia force au nguvu nyingi sana kumfanya aendelee kubaki hatimae imeshindikana,inaonekana wapo wengi sana ambao mnalazimisha waendelee kuwepo hapo kwa lazima ipo siku mtakuja kufunguka wenyewe,jifanyieni tathimin timu inaelekea shimoni nafasi ya pili pia hamuipati,mtafungwa gemu moja na mtapata suluhu moja ina maana mtapoteza alama 5 kati ka 15 mlizobakisha,yani atafungwa na simba na atasuluhu na dodoma,jumla atakua na alama (61+10=71),azama atasuluhu mechi mbili mechi ya simba na mechi na namungo,jumla atakua na alama(60+11=71),magoli mtakayofungwa na simba ndiyo yatakayowaponza mkose klabu bingwa Afrika msimu ujao.ukichanganya na jeuri zenu ndio kabisaaa.kwa maana hiyo simba anatafuta alama 6tu asepe na ndoo.ingawa ni ngumu kuamin ila ndivyo itakavyokua.

      Delete
    2. Duuuh!! Sasa ndugu yangu isha ndeeefu mpaka inachosha unaongea usilolijua kuhusu Yanga,si bora ungekaa kimya uwe na uelewa wako usio na mashiko. Muda mwingine uwe unajitathmin binafsi

      Delete
  6. Kama hawata jirekebisha Tunapoelekea Hakutakuwa na utani wa jadi,ila kutakua na uhasama mwanzo mwisho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic