June 16, 2021


 KLABU ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila leo Juni 16 ikiwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma imeyeyusha pointi tatu mazima baada ya ubao kusoma JKT Tanzania 2-0 Ihefu FC.

Ni Jabir Aziz alimtungua kipa namba moja Deogratius Munish, 'Dida; dakika ya 3 kwa pigo huru na bao la pili lilipachikwa kwa kichwa cha Edson Katanga dakika ya 8.

Matokeo hayo yanaifanya Ihefu ibaki na pointi zake 34 ikiwa nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi 31 na JKT Tanzania inafikisha pointi 36 ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 31.

Pia Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza ikiwa Uwanja wa Kaitaba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons. Ni Yusuph Mhilu alipachika bao hilo kwa kichwa dakika ya 44.

Kwa ushindi huo Kagera Sugar inafikisha pointi 36 nafasi ya 11 huku Prisons ikiwa na pointi zake 41 nafasi ya 8.

1 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi kweli kiazi. Sisi tumeona Yusuf Mhilu akifunga kwa mguu wa Julia Wewe unatuambia kafunga kwa kichwa. Uliangalia mechi au umehadithiwa? acha uongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic