June 5, 2021


 KOCHA Mkuu wa Namungo FC ya mkoani Lindi, 
Hemed Morocco, amefunguka kwa sasa anajikita kukisuka upya kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ili kurudi kwenye makali yake kama msimu uliopita.


Namungo FC inapambana kuhakikisha inamaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ili wawe na nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Msimu huu katika Kombe la Shirikisho imeishia hatua ya robo fainali baada ya kutupwa nje kwenye hatua hiyo (ASFC) na Biashara United kwenye mchezo uliopigwa Mei 23 mjini Musoma.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Morocco

alisema: “Kwa kiasi kikubwa timu imetumika sana na wachezaji wamechoka kutokana na kushiriki mashindano mengi msimu huu, kwa sasa tunajikita kumalizia mechi zetu za ligi zilizobaki ili tuweze kujiandaa na msimu ujao.


“Malengo yangu ni kukisuka upya kikosi ili tuweze kufanya vizuri msimu ujao kama ilivyokuwa msimu uliopita, nitafanya maboresho kadhaa kwenye maeneo mbalimbali ndani ya kikosi ili tupate kikosi bora chenye uwezo wa kupambana kwenye kila michuano ambayo tutashiriki.”


Namungo FC inashika nafasi ya nane kwenye

msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41

baada ya kushuka dimbani kwenye mechi 30

wakishinda mechi 10, sare 11 na wamepoteza

mechi tisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic