June 8, 2021

 


WAKATI timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ikiwa imeanza mazoezi jina la kiungo Bryson Raphael mali ya Azam FC limeondolewa katika kikosi hicho.

Nyota huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji 27 walioitwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa Juni 13, Uwanja wa Mkapa.

Baada ya jina la nyota huyo kuondolewa mbadala wake ni nyota Yohana Mkomola anayekipiga ndani ya Vorskla Poltava ya Ukraine.

Taarifa kutoka kambi ya Stars zimeeleza kuwa Bryson baada ya kuwasili kambini alitoa taarifa kuwa ana majeraha ya kifundo cha mguu na kuomba aondolewe.


Chanzo: Spoti Xtra

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic